Diamond Platnumz amemtaja Vanessa Mdee kama muimbaji anayemkubali zaidi na ambaye anaona atafika mbali zaidi. Akiongea na Bong...
Diamond Platnumz amemtaja Vanessa Mdee kama muimbaji anayemkubali zaidi na ambaye anaona atafika mbali zaidi.
Akiongea na Bongo5, Diamond amesema hata jukwaani, Vanessa ni msanii anayejituma sana.
“Unajua wasanii wa kike wote wa hapa nyumbani ninawakubali ila
namkubali sana Vanessa. Na hata nikikutana naye huwa namwambia kuwa
‘Vanessa unanipa imani sana kuwa tuna mwanamuziki wa kike ambaye naona
kabisa anabadilika kila siku na anajituma sana hata akiwa kwenye stage’.
Unaona kabisa ana juhudi zaidi maana Vanessa alikuwa akiimba kizungu
sana lakini kila siku zinavyoenda anabadilika na anaelewa nini anafanya
sio mtu wa kujitoa fahamu,” alisema.
“Kwahiyo nina imani ipo siku tutaona msanii wa kike kutoka Tanzania
anafanya vizuri. Kwahiyo Vanessa namkubali sana na nina imani atafika
mbali, ni mfano mzuri sana pia na kwa wengine kujituma zaidi na kuwa
wabunifu wa kazi.”