YAHAYA unaishi wapi? Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya...
YAHAYA unaishi wapi? Jamaa mmoja anayetumia majina ya Baraka, Muba au Martha Peter amenaswa kwa kujipatia pesa kiudanganyifu akijifanya Ofisa wa Bodi ya Mikopo wa Chuo cha Ardhi kilichopo jijini Dar.
Akizungumza na waandishi wetu, Wema alisema alimfahamu tapeli huyo kupitia kwa rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Rebecca, ambaye naye awali alipigiwa simu na mtu huyohuyo akimtaka kimapenzi.
Wema alisema kuwa rafiki yake alimkatalia tapeli huyo, lakini siku chache baadaye alimpigia tena akimwambia kulikuwa na nafasi ya kazi katika Chuo cha Ardhi hivyo anamhitaji yeye kwa ajili ya nafasi hiyo.
“Kwa sababu Rebecca ana kazi yake tayari
aliamua kunitaarifu mimi kwa kuwa anajua natafuta kazi,” alisema
Wema.Alisema alikutana na jamaa huyo ndani ya Chuo cha Ardhi na kupatiwa
fomu aliyoelekezwa kujaza kisha akatakiwa kutoa shilingi 280,000 kama
malipo ya fomu hiyo na gharama za mafunzo ya siku tatu ya vitendo kuhusu
kazi, fedha ambazo hakuwa nazo kwa muda huo na kulazimika kumuomba
rafiki yake Rebecca amsaidie.
Katika Kituo cha Afya Kimara, alikutana tena na tapeli wake, aliyeonekana kuwasalimia madaktari na manesi kana kwamba wanajuana kisha akaingia kwa dokta na kuzungumza naye.Baada ya muda tapeli huyo alitoka nje kisha akamwambie Wema aingie kwa daktari kwa ajili ya kujaziwa fomu hizo kienyeji bila kupimwa maambukizi ya ukimwi.
“Nikiwa ndani machale yalinicheza, ikibidi nimuulize yule daktari kama anajuana na yule jamaa, daktari akasema kwamba hawafahamiani hata kidogo jambo lililonishtua. “Nikamnong’oneza kuwa nahisi kutapeliwa, akaniambia nikakae naye nikijifanya namuongelesha huku yeye akizunguka kwa mlango wa nyuma na kuwaita mapolisi.
“Polisi walichukua maelezo yangu na kufungua jalada RB/4969/2014 KUJIPATIA PESA KIUDANGANYIFU kisha wakaniambia nifike kesho yake,” alisema Wema na kuongeza kuwa siku ya pili alipofika kituoni hapo aliwakuta watu wengine waliodai kutapeliwa na jamaa huyo kwa majina tofauti na walipopiga hesabu fedha alizowatapeli kwa pamoja zilifikia sh.1,435,000.