post-feature-image
HomeBurudani

Huyu Ndio baba Haji, msanii wa filamu anayewekeza kwenye elimu- Mtambue Sasa.

Anafikiria mbali zaidi BABA HAJI kama anavyojulikana mtaani kwa sasa au tuseme Baba Jamila amezaliwa Okto...

Kala Afunguka na kusema "Mwaka huu nimeingiza kipato kikubwa kuliko miaka yote" Pia Akanusha kupotea kwenye game
Baada ya Kumkimbia Mumewe, Aunt Ezekiel Adungwa Mimba na Mume wa Mtu
HATIMAYE CHID BENZ APATA DHAMANA KATIKA KESI YA MADAWA YA KULEVYA
BABA HAJI kama anavyojulikana mtaani kwa sasa au tuseme Baba Jamila amezaliwa Oktoba 11,1980 katika kijiji cha Sakura wilaya ya Pangani mkoani Tanga na kupewa jina la Haji Adam. Baba Haji yeye ni muigizaji filamu. Anajulikana sana kwa sinema zake za Miss Bongo, Saa 24,Babra, Sandra na  inayotamba sasa hivi ya Jamila na Pete ya Ajabu.

Haji Adam kama nilivyosema amezaliwa kutoka kwa mama mkulima na baba dereva wa magari makubwa katika kijiji cha sakura akasomea hukohuko na kuja dar es salaam kuwafuata wazazi wake baada ya baba yake ambaye alikuwa anafanyakazi kampuni ya kinywaji ya Tanzania Breweries kupata uhamisho. Alifika Dar es salaam akiwa amemaliza darasa la saba mwaka 1992 shule ya Kipumbwi na kujiunga na Sekondari ya Jitegemee mwaka 1993 alikomaliza kidato cha nne.

Unaweza kusema kwamba ni mmojawapo ya waigizaji waliojipeleka shule kusomea masuala ya uigizaji katika chuo cha sanaa Bagamoyo ambako  wakati wa kuchukua diploma yake alitumikia serikali ya wanafunzi wa hapo mkwanza kama waziri na kisha rais wa serikali ya chuo.

Kwa sasa anajipanga kwenda Chuo kikuu na ameanzisha kampuni yake ya filamu iliyoanza mwezi uliopita ikijulikana kama HAPA PRODUCTION.

Baba Haji alianza shughuli za kuigiza miaka ya 2000 baada ya kuingizwa katika kundi la akina Monalisa.
katika mahojiano alisema kwamba akiwa anafanyakazi ya kuhudumu pampu katikam kituoc ha mafuta mama John mkoani Mbeya  walifika Monalisa na mama yake,Natasha,  wakati wa kipindi cha Bingo wakataka watu wa kuigiza katika steji akajikurupusha akaingia na kufanya kweli na hivyo kuitwa Dar es salaam.

Alipofikia Dar es salaam kama alivyoagizwa katika maeneo ya Mikocheni  Tanesco alikutana na Natasha na Marehemu George Tyson ambaye walizungumza na kisha kumwelekeza katika kasting iliyofanyika ukukmbi wa Utamaduni wa watu wa Urusi.

Huko alikutana na pia na akina Ritch, mjomba Fujo ambao walimpa kazi ya kumeza kitabu cha Mkaguzi wa serikali  kilichoandikwa na Nikolai Gogol mwaka 1880. Alipewa siku nne kukamilisha kazi hiyo na aliikamilisha.

Kitabu hicho kilitakiwa kuigizwa katika maonesho ya ZIFF ya mwaka 2000.

Hata hivyo kazi yake ya kwanza ilikuwa ushiriki wake katika tamthilia ya Ndoto iliyokuwa inarushwa katika televisheni ya CTN ambako ndiko alikopatia jina la Baba Haji.

maisha ya mapema
Mtoto wake wa Pili

Adam ambaye ana ndugu saba na yeye kuzaliwa wa nne na kuigiza filamu takaribani 30 sasa amesema kwamba baada ya kumaliza shule ya Jitegemee, alianza kazi katika mkituo cha mafuta cha Ukonga Madafu cha Nassoro Filling Station mwaka 19978 na mwaka 1998  alihamishiwa Mbeya kituo cha Agip cha Mama John.

Mwaka 2000 pamoja na mafanikio yake alichukia kazi na hata walipofika wageni kutoka dar es salaam na kipindi chao cha Bingo alifanya mazungumzo na kuja Dar es salaam ambako walimuingiza katika kundi lao.

Kundi la akina Natasha ambako aliingizwa liliyumba wakati wakisubiri kamera kurudi kutoka matengenezoni Kenya ndiupo Single Mtambalike na yeye walipotoka na kuanzisha kundi la Kamanda Familuy maskani yakiwa Ilala.

Wakati wanaenda Ilala, CCM ilikuwa inaongozwa na Mikidadi Mahmood na katibu wake Rajab Kundya. Viongozi hao wa CCM waliwapokea na wao wakaanza kufanya mazoezi ya kuigiza.

Wakiwa hapo jndipo wao walipompatia Emmanuel Nchimbi fomu ya kugombea uenyekiti wa UVCCM Taifa 2004 na kuupata.

Wakati filamu zinashika kasi nchini (bongo Movie) mwaka 2005 kundi la Kamanda nalo likayumba na yeye akajitoa na kuanza kufanyakazi binafsi.

Kuyumba kwa kundi hilo kulitokana na yeye kupata nafasi ya kwenda kuigiuza katika filamu ya Tumaini ambayo ilitwaa tuzo katika tamasha la ZIFF.

Filamu ya Tumaini ambayo iliigizwa kwa takribani  mwezi mmoja wilayani Muleba ilipokamilika na yeye kurejea Dar es salaam kundi lilisambaratika na hasa kwa kuwa Mtambalike alikuwa kazini na yeye hakuwepo.

Baba Haji  alipoingia katika sinema alikuwa tayari na mke ambaye amezaa naye watoto wawili ambapo mmoja mkubwa yupo sekondari na wa pili ana miaka miwili na nusu. Kwa sasa hayuko na mke wake huyo ambaye anasema kwamba alimuoa akiwa na umri mdogo.

kwa sasa anaishi na mchumba ambaye anaamini kwamba wanakwenda vyema kwa kuwa wote wawili wanashabikia vitu vinavyofanana tofauti na wa kwanza ambaye alikuwa anataka kuua mapenzi ya kazi ya uigizaji.
kazi zake
Mtoto wake wa kwanza
Haji anasema kwa muda sasa anafanya kazi za wengine, akitarajia kuitumia kampuni yake vyema ili kufanyakazi zake. Akiwa anapenda sinema za aksheni amejikuta akiigiza sinema za masimulizi kutokana na kile alichosema kukosekana kwa wataalamu wa kuandika skripti za aksheni.

Alisema kwa sasa taifa hili halina tatizo la vipaji bali waandishi wa skripti ambao mara nyingine wamekuwa wakjigonganisha mawazo na kutoa sinema zinazofanana.

Mwaka huu Baba Haji amesema kwamba  ametoka na sinema za watu kama Kwanini mama, jamila na pete ya ajabu, who is my Child na kitendawili.

Sinema zote hizo ni masimulizi na si za aksheni lakini zimepata mashabiki wake.

katika sinema hizo, mradi uliompa hekaheka ni wa Jamila kutokana na moja ya vipande kutumiqa saa takaribai 10 huku wakiwa na flashba zipatazo 40 ndani ya tukio moja.

Alisema pamoja na kuongeza uwezo kupitia elimu aliyoipata Bagamoyo, shida anayoiona ni  baadhi ya madairekta kutofuata ushauri unaofaa hasa katika kuwa kioo cha jamii yaani kutoa mafunzo katika sinema zinazoigizwa.

Alisema ipo haja  sinema za Tanzania zikabadilika kuwa za watu wa chini badala ya kati ambao pia hawachangii katika maendeleo yake na kwamba tabia za kukopi hapa na pale na kutengeneza sinema zinawaondoa watanzania katika uhalisia na hivyo kushindwa kufanya masimulizi yao yanawaonesha wao ni kina nani.

Anasema pamoja na utamu wa filamu ya Jamila yapo mengi ya kujifunza kama muigizaji, mambo ambayo anasema yanahitaji tu upeo mkubwa wa elimu katika sanaa hiyo.

Anasema kutokana na ukweli huo anakwenda kuongeza elimu ya Chuo Kikuu akijiorodhesha katika chuo kikuu cha Dar es salaam kusomea perfoming art.

Mimi naona elimu ni bima ya maisha na ngazi ya mafanikio.

Adam ni msanii binafsi ambaye amekuwa akiongeza ujuzi kwa kusoma. Alianzia Bagamoyo akajisomesha kwa kupitia filamu na hata Chuo Kikuu  atajisomesha kwa staili hiyo hiyo.

Akiwa mwanafunzi wa Bagamoyo 2010 hadi 2013 amejisomesha mwenyewe kutokana na filamu akitumia siku za Ijumaa Jumamosi na Jumapili kufanyakazi za watu na kurejea darasani Jumatatu na anasema atakwenda staili hiyo kukamilisha digrii yake.

Gharama za masomo zilikuwa milioni 6.5 ukiachia gharama nyingine na akiwa hapo alikuwa Waziri wa habari, utamaduni na michezo na baadae urais wa serikali  ya chuo.

Amesema kwamba anachofikiri sana ni namna ya kuwapatia watu sinema zao kwa kuangalia simulizi za hapa nyumbani  kwa kupitia kampuni yake ya HAPA PRODUCTION iliyoanza Agosti 6,2014. Ni matarajio yake kwamba kampuni yake itakuwa kubwa Afrika Mashariki itaklayozalisha mahitaji ya watu.

"Tazama sinema ya kigodoro ni mbovu kabisa, lakini simulizi lake lililojaa uswazi limeipa shavu kubwa" alisema  Adam na kuongeza kuwa filamu za aina hiyo zimepewa heshima kubwa katika akili yake na kutaka kuzifanya kitaalamu zaidi.

 Kero zake

Ana kerwa na vitu vingi katika tasnia ya filamu. Kitu kimoja kinachomkera sana ni matangazo ambapo ili mtu apande lazima afanye kashifa.Anadhani atakuwa kama akina Mel Gibson  na Bruce Wills ambao kazi zao ndio zinazuza lakini si  kashifa. Tatizo la pili ni kukosekanaa kwa waandishi wa skripiti na tatu ni kukopi na kupesti kunakofanywa na watunzi wa filamu.

Anasema mwandishi kwa mkupuo mmoja anaandikia sinema zaidi ya saba hali inayoondoa uhalisia na pia kuzifanya sinema kufanana mno bila sababu huku zikitolewa na kampuni tofauti.

Pia anasema tabia ya kuchakachua sinema za Kihindi na Nigeria kupata filamu inayodaiwa ya kitanzania inamnyima raha kwani anaona visa vya kitanzania haviongeleki bali visa vya kufikirika kutoka katika sinema za kihindi au Kinaijeria.

Anasema hali ya baadae ya sinema za kitanzania ni mbaya kama hakutokei maamuzi ya makusudi ya kutumia visa vya tanzania na hasa wasomi katika vyuo kutoka katika kazi zao na kushiriki kuandika miswada mbalimbali.

Anasema pamoja na ukweli kuwa vipaji vipo nchini waigizaji ahwaishi katika uhusika wa mtu na kujikuta wakiwa wabangaizaji badala ya kuwa waigizaji.
Na katika hili amemsifu sana Mzee majuto katika kuwezesha uhasilia wa watu anaowaigiza.

Maisha yake

Ingawa alioa akiwa na miaka 18 baada ya kujiona ana fedha japo baba yake alimzuia akimtaka afikishe miaka 34 ndio aoe, amesema ni matumaini yake kwamba mchumba aliyempata sasa hivi ambaye anatoka Nyanda za Juu Kusini bibie Latifa Sharj atakuwa wake daima kutokana na kulingana katika mambo yao.
"Nisemeje wa kwanza alikuwa hataki kabisa nifanye kazi ya uigizaji , huyu wa sasa ni shabiki yangu huku akinisaidia kutoka kikwelikweli katika mitoko mbalimbali ya kazi zangu" alisema Adam ambaye watoto wake Adam (13) na Tareq ambaye alimpa jina kutokana na kumhusudu Tareq Aziz na mambo yake wakiwa kumbukumbu jema la baba anayetafuta maisha bora kwa wanawe.
Anasema baba na mama yake wako hai na bado anakumbuka sana maneno ya baba yake ya kupevuka kwanza ndio kuoa.
Anasema anapenda muziki Live na muziki wa taarabu.
Anawaomba watanzania kusaidia kukuza sanaa kw akuwa wazalendo kununua kazi za wasanii na kuangalia sinema za Kitanzania, kuzikosoa na kuzipa mwelekeo adilifu wa kitamaduni.
Pamoja na kauli hiyo amesema wakati umefika kwa madairekta kulenga sinema za Tandale na kuacha watu wa masaki.
source:Beda msimbe ilitoka mara ya kwanza Habarileo Jumapili Septemba7,2014
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: Huyu Ndio baba Haji, msanii wa filamu anayewekeza kwenye elimu- Mtambue Sasa.
Huyu Ndio baba Haji, msanii wa filamu anayewekeza kwenye elimu- Mtambue Sasa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3AMbkAB6JX20-W-RatG2ifw55Q1nfnh5ZMVW8vKgbukiQttkWeTJBMqTrmwNWLHxq_YAHZykbDg6BlHyo9iqM81IOkeZV4IOztbgy8KJqi-nFwKBK-6XxfPMtYSjdAwNQFA3dUetHHCo/s640/babahaj3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3AMbkAB6JX20-W-RatG2ifw55Q1nfnh5ZMVW8vKgbukiQttkWeTJBMqTrmwNWLHxq_YAHZykbDg6BlHyo9iqM81IOkeZV4IOztbgy8KJqi-nFwKBK-6XxfPMtYSjdAwNQFA3dUetHHCo/s72-c/babahaj3.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/huyu-ndio-baba-haji-msanii-wa-filamu.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/huyu-ndio-baba-haji-msanii-wa-filamu.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago