Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amedai kuwa amezunguka katika nchini kibao duni...
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya
amedai kuwa amezunguka katika nchini kibao duniani lakini hajawahi kuona
nchi yenye wasanii wa Hip Hop fake kama wa Tanzania.
Akizungumza jana, Dudu amesema aliwahi kujaribu kukutana na
baadhi ya wasanii wa Hip Hop na kujadili baadhi ya changamoto zao ila
ziligonga ukuta kutokana na uoga wao.
“Nimezunguka dunia nzima sijaona nchi yenye wana Hip Hop fake kama
Tanzania,” amesema Dudu. “Yaani wana Hip Hop wa Tanzania ni fake, yaani
hawajui maaana ya Hip Hop. Nilishawatafuta wengi tufanye harakati za
kuokoa muziki wetu lakini nikiwafuata wanasema ‘aise bro hizi harakati
ni ngumu’. Kama utakuwa unaona hata kutafuta haki yako ni ngumu utakufa
ukiwa masikini kutokana na dosari za uzembe. Wewe unatakiwa uitetee
jamii halafu unaogopa watu kwanini sasa uitwe mwana Hip Hop?
Nilishawafuata wasinii wengi wa Hip Hop tutengeneze structure ya muziki
wetu kibiashara lakini hawaeleweki. Nilishamfuata Professor, nilishakaa
na Mwana FA, na nimeshakaa na wasanii wote wa Hip Hop unaowajua lakini
wananiambia ‘bro hizi harakati zako hatuziwezi’,” amesema rapper huyo.
Katika hatua nyingine Dudu Baya amewataka wanawake wote ambao ni
wadau kwenye burudani kuwasaidia wasanii wa kike wanaohitaji msaada.
“Unajua wanawake wanateseka sana kwenye hizi harakati za muziki wetu,
tunahitaji kuwasaidia, kwa sababu presenter ili aicheze ngoma yake
anahitaji kutoa rushwa ya ngono, producer pia, waandishi. Kwahiyo
kiukweli wasanii wa kike wanahitaji kusaidiwa na wadau wa kike ambao
wapo kwenye huu mtandao wa muziki. Kuna watangazaji kama akina DJ Fetty
wapo wengi. Hao ndo wanatakiwa kuanzisha harakati za kuwasaidia wasanii
wa kike. Nipo kwenye mchakato wa kuzungumza na baadhi ya wadau ili tujue
tunajadili vipi ili kuwasaidia hawa ndugu zetu.”