Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata m...
Katika
hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini
linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya
msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana
ngono.
Kuna
watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku
wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au
tatu.
Mtu
anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia
‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na
kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.
Hilo
linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini
uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu
wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika
kundi la watu wapenda ngono.
Pamoja
na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu
asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana
nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa
kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila
tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti
kwa vile tu miili imetaka kufurahika.
Twende pamoja katika kutazama madhara hayo kwa kina.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO.
Watu
wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za
kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za
kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa
tendo la ndoa mara kwa mara.
Sababu
hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza
kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.
Aidha
kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza
kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za
mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba
kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione
jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye
na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa
kikamilifu.
KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA.
Tabia
ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa
homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa
kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na
hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia
tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na
kwa wakati gani?
Watu
wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara
ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani
bila kujali hadhi yake.
Hawa
ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa
ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa
vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.
Unapokuwa
mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na
uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili
unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.
KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO.
Raha
ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na
mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi
ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza
msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo
haikutoshi kumaliza tamaa yako.
Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!
KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI.
Madhara
mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara
kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.
Kama
tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya
watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha
lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa
nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.
Sambamba
na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya
mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.
KUPATA MAGONJWA.
Kama
tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa
mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela
ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo
ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa
kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na
kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza
kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo
kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya
haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.