Muigizaji wa filamu wa Marekani, Gabrielle Union na mchezaji wa NBA, Dwyane Wade waliofunga ndoa hivi karibuni, wametua Tanzania kwaajil...
Muigizaji wa filamu wa Marekani, Gabrielle Union na mchezaji wa
NBA, Dwyane Wade waliofunga ndoa hivi karibuni, wametua Tanzania
kwaajili ya honeymoon.
Mastaa hao waliofunga ndoa Aug. 30, wamekuwa wakishare picha kwenye
mtandao wa Instagram zinazonesha bata wanazokula kwenye fungate lao
katika maeneo mengi duniani. “When the Indian Ocean is ya swimming pool…
You dive in! But first… Play that @beyonce baby,” Union, 41, aliandika
kwenye Instagram.
Wakiwa Tanzania, jana wawili hao walitembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti na kupiga picha na wamasai kadhaa.
“Pure joy! Life on the Serengeti… #Tanzania #Masai #2ndLeg … I emoji️
the photographer #BrianFellows,” ameandika Union kwenye picha hiyo.