Archive Pages Design$type=blogging

Filamu ya Tanzania ‘Dogo Masai’ kuwania tuzo nchini Marekani

Filamu ya Kitanzania iitwayo ‘Dogo Masai’, imetajwa kuwania tuzo za Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) za nchini Marekani. Fil...

fawerryFilamu ya Kitanzania iitwayo ‘Dogo Masai’, imetajwa kuwania tuzo za Silicon Valley African Film Festival (SVAFF) za nchini Marekani. Filamu hiyo imetayarishwa na kuongozwa Timoth Conrad Kachumia, wa Timamu African Media.

 
Dogo Masai imeingia kwenye kipengele cha Best Feature Film ambapo inashindana na filamu kutoka katika nchi mbali mbali zikiwemo Afrika Kusini, Malawi, Misri, Nigeria, pamoja na Uganda. “Kutoka nchini Tanzania Dogo Masai ni filamu pekee ambayo imeingia kwenye mashindano hayo, lakini kwa East Africa ni filamu mbili ambayo moja ni kutoka Uganda na hapa kwetu,” amesema Timoth.
Kuona list nzima ya filamu zilizochaguliwa kushindana na DOGO MASAI fungua mtandao hapa.
Licha ya kufanikiwa kuingia kwenye tuzo hizo za Marekani, lakini pia Filamu hiy imechaguiwa kuingia kwenye tamasha la Rome Independent Film Festival (RIFF) la nchini Italia.
Si mara ya kwanza kwa Timoth kuandaa filamu ikaingia kwenye tuzo kubwa barani Ulaya. Mwaka mwaka jana Timoth Conrad alihusika katika kuandaa filamu iliyoitwa Mdundiko iliyoongozwa na Jackson Kabirigi. Nayo ilileta heshima nchini baada ya kufanikiwa kunyakua tuzo hizo za SVAFF ambazo zinaandaliwa nchini Marekani. Licha ya kunyakua tuzo hizo lakini pia ni filamu ambayo ilipata nafasi ya kuchaguliwa kushindana kwenye tuzo nyingi barani Africa na kwingineko.
DOGO MASAI ni filamu ya kitanzania inayomuelezea kijana Dogo masai ambaye anaamua kuuvaa uhusika wa kuwa muonekano wa kimasai baada ya kufanyiwa vitendo vya kinyama na mjomba wake. Hivyo anaingia katika safari ndefu ya kutafuta suluhisho la yote aliyofanyiwa. Ni filamu ya kusisimua na kuhuzunisha pia kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao Dogo Masai.
Wahusika kwenye filamu hiyo ni pamoja na Omary Clayton, Hissani Muya, Mainda Suka, Julieth Samson na Mukasa Tabani.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: Filamu ya Tanzania ‘Dogo Masai’ kuwania tuzo nchini Marekani
Filamu ya Tanzania ‘Dogo Masai’ kuwania tuzo nchini Marekani
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/09/fawerry.jpg
https://i.ytimg.com/vi/gyemmaw4x_A/default.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/filamu-ya-tanzania-dogo-masai-kuwania.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/09/filamu-ya-tanzania-dogo-masai-kuwania.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago