Diamond Platnumz amerejea tena kwenye msimu wa pili wa kipindi cha Coke Studio Africa na awamu hii atatangeneza pair na hitmaker wa John...
Diamond Platnumz amerejea tena kwenye msimu wa pili wa kipindi
cha Coke Studio Africa na awamu hii atatangeneza pair na hitmaker wa
Johny, Yemi Alade kutoka nchini Nigeria.
Diamond ni msanii wa nne mwaka huu kutoka Tanzania aliyeshiriki
kwenye kipindi hicho kinachorekodiwa jijini Nairobi, Kenya. Wengine ni
Vanessa Mdee aliyerekodi na Burna Boy wa Nigeria, Joh Makini aliyerekodi
na Chidinma wa Nigeria na Shaa aliyerekodi na Jacky Chandiru wa Uganda.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yemi aliyekuja nchini mwaka huu ameweka picha akiwa na Diamond katika studio hizo na kuandika: #wonderment! With the infamous ubertalented six-abbs superstar Diamond….@diamondplatnumz #iAmHumbled #thankYouCokeStudio, ForThe Opportunity God bless AFrica.. #cokeastudioafrica @cokestudioafrica @dresomes Nosa @chocolatecity Diamond has been singing your song all morning @audumaikori.
Naye Diamond katika picha akiwa na mrembo huyo ameandika:
Na dem ake Johny @yemialade , ushaelewa nini kinaendelea si
eti????….. (jus me and Johny’s Girlfriend…You allready know what it is
ryt???… Cc @yemialade
Diamond na Yemi Alade wakipewa maelekezo