Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba Sehemu ya ukumb...

Gari ya Polili ilioibuka kumuokoa Diambond kufuatia sakata la mashabiki wake kupandwa na jazba

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini stuttgart,ujerumani
UJERUMANI SI SHWARI KIMENUKA !!
POLISI UJERUMANI WAMUOKOA DIAMOND KUTOKA KWA WASHABIKI WENYE HASIRA ! KASHINDWA KUWIKA STUTTGART KISA ?
KAFIKA UKUMBINI SAA 10 ALFAJIRI ! WASHABIKI WANASUBIRI SHOW TANGU SAA 4 USIKU
PROMOTA MNAIJERIA AINGIA MITINI ,DJ APATA KISAGO HETI VYOMBO VIBOVU ! AIBU
Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe 30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika
hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,ujerumani,baada
ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show,washabiki hao
waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya
saa10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na
promota wake raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.
Hapo
ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha
chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,Kilichowakera
zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi
huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muzikima-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ Flor
alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao
walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. Polisi nchini
ujerumani wanamesema tukio hili la haibu alijawahi kutokea,kuwa msanii
kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari kwani
washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwawanachunguza
thamani ya hasara hiliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia
mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa
kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wa hasira nawe DIAMOND" link: