Mwanamuziki kiongozi wa bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Baba, akiwa na mkewe. Stori: Shakoor Jongo MWANAMUZIKI ...
Mwanamuziki kiongozi wa bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Baba, akiwa na mkewe.
Stori: Shakoor Jongo
MWANAMUZIKI kiongozi wa bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Baba, maarufu kama Chalz Baba, ambaye wiki iliyopita alimpa kipigo kikali mkewe, Rehema Sospeter na kusababisha ndoa yao kuyumba, hatimaye amemuomba radhi na hivi sasa wawili hao wamerejea kwenye uhusiano wao kama awali.
Ilidaiwa kwamba baada ya tukio hilo, hata hali ya kiongozi huyo wa bendi haikuwa nzuri kisaikolojia, jambo lililofanya uongozi wa Mashujaa kuamua kuingilia kati ili kuiokoa ndoa hiyo.
Mmiliki wa Mashujaa Musica anayejulikana zaidi kwa jina la Mamaa Sakina, ndiye aliyefanya shughuli hiyo ya kusawazisha mambo kabla hayajaharibika zaidi.
Risasi Mchanganyiko lilifanikiwa kukutana na Mamaa Sakina katika ukumbi wa Ten Lounge uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam akiwa amekaa na mke wa mwimbaji huyo. Muda mchache baadaye Chalz Baba pia alitokea na moja kwa moja aliongoza kuelekea meza aliyokaa mkurugenzi huyo.
Chalz Baba,
“Ni kweli kabisa kama ulivyosikia, kwa sasa mimi na mke wangu
tumemaliza tofauti zetu, nimemuomba radhi amenielewa, ile ahadi yake ya
kutaka nimrudishe kwao ameifuta na sasa hivi tumeanza upya maisha yetu
ya ndoa,” alisema Chalz Baba.Naye kwa upande wake, Mamaa Sakina alisema anamshukuru Mungu kuona ndoa hiyo imerejea kwani isingekuwa vizuri kuona imevunjika.“Sasa hivi Chalz na mkewe kama unavyowaona, mahaba tele wamemaliza tofauti zao,” alisema.
SAJENTI NUSURA ATIBUE HALI YA HEWA
Wakati mambo yakionekana kunyooka, ghafla hali nusura ibadilike baada ya zilipendwa wa Chalz ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja wa kike anayejulikana kwa jina la Husna Idd ‘Sajenti’ kwenda mbele kumtunza mwanamuziki huyo alipokuwa akifanya makamuzi jukwaani.
Kitendo hicho kilidaiwa kumuudhi Rehema ambaye alijikuta akinuna ghafla hasa baada ya Chalz kutabasamu kwa kutunzwa na Sajenti.