Young Killer amesema ametumia gharama kubwa kufanikisha kushoot video ya wimbo wake ‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro. ...
Young Killer amesema ametumia gharama kubwa kufanikisha kushoot video ya wimbo wake ‘Umebadilika’ aliomshirikisha Banana Zorro.
Killer amesema kuwa zaidi ya shilingi milioni nane
zimetumika hadi kuikamilisha. “Ni video ambayo nimeingia gharama kubwa,
tofauti na video zote nilizowahi kuzifanya,” amesema rapper huyo. “Yaani
ukianza kulinganisha video zangu ambazo zimepita nadhani kwa hii video
inafikia katika maandalizi tu yaani sio hela ya kumlipa director ni kama
milioni nne.”
Young Killer amesema ili kwenda kushoot video hiyo kisiwani Mbudya ilimlazimu kukodi boti kwa siku mbili.
“Hiyo ni kwenye mtumbwi tu, bado kuna ngalawa mle, tulikodisha
ngalawa kushoot sehemu za Banana. Kuna watu waliocheza mle wamehitajika
kulipwa, kuna majengo ya zamani tuliyakodisha, nauli za hapa na pale,
watu wanahitaji wale,” ameongeza.
Rapper huyo amesema video hiyo ni kali kuliko hata anavyoisema
mdomoni. “Naamini watakayoiona itakuwa kali zaidi ya hii ninayoisema.”