Muungano wa wasanii wawili wacheshi na wenye vituko kutoka Kigoma, Peter Msechu na Baba Levo hivi sasa utakuwa ...
Muungano wa wasanii wawili wacheshi na wenye vituko kutoka
Kigoma, Peter Msechu na Baba Levo hivi sasa utakuwa ukitambulika kwa
jina moja la ‘2mbili Wa Town’.
Wasanii hao ambao ukibahatika kukutana nao ni ngumu kuondoka bila
kuvunja mbavu zako, wanatarajia kutambulisha project yao mpya ya pamoja
ya ‘2mbili wa Town’ hivi karibuni.
“Jina la project linaitwa Tumbili wa town, so kuna vitu vingi ndani ya hiyo project, sema bado hatujaamua kuielezea project nzima mambo yake ya ndani na vitu vilivyo kwasababu kuna mshindo mkubwa unakuja wakati wa kutambulisha hiyo project.” Baba Levo ameongea leo

Baba Levo amesema ‘Tumbili Wa Town’ ni kundi la watu wawili yeye na Peter Msechu litakalokuwa likifanya mambo mengi.
“Kwanza kwa kifupi ni kama kundi, ni kundi la watu wawili sema
sasa kuna vitu ambavyo tutakuja kuvifanya ambavyo ni vitu vikubwa sana
sana kwenye hii industry ya muziki, movie na vitu kama hivyo. So ni
kwasababu hatujakuwa rasmi kwaajili ya kuielezea hiyo project ndio maana
unaona tunakuwa tunaielezea juu juu , kutokana na watu wanaoisimamia
project kusema wanataka wahakikishe vitu vyote vimekaa sawa sawa and
then sasa ndio tuitambulishe watu wote wajue ni kitu gani,” alisema Baba Levo.
Ameongeza kuwa licha ya kuungana na Peter Msechu kwaajili ya project
hiyo lakini kila mmoja bado ataendelea na project zake binafsi za muziki
walizokuwa wakizifanya toka zamani.
“Hii project haiwezi kutufanya tusiendelee na project zetu ambazo tumekuwa nazo kuanzia mwanzo, bado tutaendelea kuwa na brand zetu zile zile kama Baba Levo, kama Peter Msechu lakini kwa pamoja tunatengeneza Tumbili Wa Town”.

Naye Peter Msechu kupitia Instagram aliandika kuhusu project hiyo:
“and our official name is “2MBILI WA TOWN” more project to come ya all stay tuned…. we on point this year no jokes at all… wengine mnatutukana ni sawa tunashukuru wengine mnafurahi tunachokifanya pia tunawashukuru.. tunachoamini ni kila mmoja anajua namna anavyo tafuta ugali wake.. hii ni yetu ili mradi hatuibi wala kukaba mtu basi tunamshukuru Mungu..”

Baba Levo alimaliza kwa kusema kuwa ndani ya wiki mbili au tatu zijazo project ya Tumbili Wa Town itatambulishwa.