Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufany...
Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi
kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa
ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.
Akiongea kupitia kipindic ha The Chart ya 100.5 Times Fm
kinachoongozwa na Jayree, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema
kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaaada mkubwa katika nyimbo zao
zote.
“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer
alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo
yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio
tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa
tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri.
Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada
ya moja.” Amesema Asley.
“Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea
ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu
kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi
yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini
maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.
Wimbo wa Nitajuta wa Yamoto Band umeshika nafasi ya pili kwenye The Chart ya 100.5 Times Fm wiki hii.
Kipindi cha The Chart kinakuwa hewani kila Jumamosi kuanzia saa nne
kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana. Unaweza kusikiliza online
kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.