Tumekwisha! Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata ambao si riziki (mashoga) na wanaw...
Tumekwisha! Taarifa ikufikie kwamba wanaume tata
ambao si riziki (mashoga) na wanawake wanaojishughulisha na mapenzi ya
jinsi moja (wasagaji) kutoka nchi mbalimbali wamefanya mkutano wao
mkubwa wa kimataifa jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.
Baadhi ya Mashoga wakipata ukodaki.
Bila kujua anazungumza na mwanahabari wetu, mmoja wao alipoulizwa
nini kinaendelea hotelini hapo, alisema mkutano huo unawahusu mashoga na
wasagaji huku akibainisha kwamba unafanywa kwa siri kubwa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba.
Baada ya kupata taarifa hizo, kachero wa Ijumaa Wikienda alizama
ndani kimafia ambapo alinasa mazungumzo ya kikao hicho, ajenda kubwa
ikiwa ni kuishinikiza serikali itambue uwepo wao hapa nchini.
Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
-GPL
Mashoga wakiandamana kudai haki zao.
Tukio hilo lililonaswa na gazeti hili lilifanyika kwa siku tatu
mfululizo mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli maarufu iliyopo
Posta jijini Dar wakitaka serikali ya Tanzania itambue na kuhalalisha
mapenzi hayo ya jinsi moja na ikiwezekana hata katiba mpya inayotaka
kuundwa sasa hivi viingizwe vipengele vinavyowahusu wao.Ili kujua kama wizara inajua kinachoendelea, gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba lakini simu yake iliita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea.
-GPL