Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afand...
Professor Jay amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.
Kupitia Instagram, Professor ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe….Amen
Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa
madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua
Malaria. Akizungumza na leo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa
madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.
“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema
Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa
Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi
nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo
kwenye wakati mgumu. Huku mazishi yatafanyika kuanzia kama saa tisa hivi
lakini bado hatutajua itakuwa wapi bado tupo kwenye mipango. Malaria
ilimchukua sana, kwa familia na watoto kwetu ni msiba mkubwa sana, yaani
ni huzuni sana,” aliongeza.