Miongoni mwa wasanii wa muziki na filamu walioonesha nia ya kutaka kuingia kwenye siasa na pengine kugombea ub...
Miongoni mwa wasanii wa muziki na filamu walioonesha nia ya
kutaka kuingia kwenye siasa na pengine kugombea ubunge ni pamoja na
msanii wa kampuni ya Leka Dutigite, Linex Sunday Mjeda.
Hivi karibuni Linex alitoa kauli ya kutaka kugombea ubunge kupitia chama kipya cha ACT ifikapo mwaka 2020
Lakini leo (Agosti 19) Linex ametoa uamuzi wake mpya juu ya kauli hiyo ya kutaka kugombea, kupitia Facebook ameandika:
“Kwa kupitia ule Msemo Unaosema Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira
ya kweli naona swala la Mimi kusema ntagombea ubunge 2020 Mungu akipenda
kila mtu amekua akilitafakali kwa mtazamo wake nachotaka kuwambia watu
ni Tunapaswa kuishi kwa ndoto na matumaini ya kufanya jambo hata liwe
Lina ugumu kiasi gani nadhani sanaa bado inanihitaji Sana so siasa badae
Sana acha nipambanie sanaa yangu kwanza na watu wangu
Nimegairi#Music#my life#My everything #wemakwaubaya”