post-feature-image
HomeBurudaniHot News

Nawaomba watu wasinikosanishe na Diamond, sina ugomvi naye - Alikiba

Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanis...

TENDO LA NGONO KWA WANAWAKE WENGI NI TIBA YA SARATANI
Kanisa lawatimua waumini walio nusu uchi
Mwanafunzi wa Kidato cha pili atoroka nyumbani kisa???
Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.
Akizungumza leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.
“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.
“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.
Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.
“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: Nawaomba watu wasinikosanishe na Diamond, sina ugomvi naye - Alikiba
Nawaomba watu wasinikosanishe na Diamond, sina ugomvi naye - Alikiba
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/07/Alikiba-Mwana-Cover-Done-Mwana-Kimasomaso.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/nawaomba-watu-wasinikosanishe-na.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/nawaomba-watu-wasinikosanishe-na.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago