‘Modo’ anayekuja kwa kasi Bongo, Hamisa Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, haoni ...
‘Modo’ anayekuja kwa kasi Bongo, Hamisa
Hassan ‘Mabeto’ amefunguka kuwa, haoni hatari kuvaa nguo za kihasara
kwani anahisi utandawazi ndiyo unamsukuma kufanya hivyo.
Akizungumzia tabia yake ya kupiga picha za nusu utupu kisha kuzitupia
mtandaoni, mrembo huyo ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Miss
Tanzania miaka iliyopita alisema: “Navaa hivi kidijitali, si unajua
tena. Mimi sioni tatizo.”
Akizungumzia suala la usagaji, Mabeto alisema, baadhi ya wanawake
wamekuwa wakimsifia sana na kuonekana kama wanaoelekea kumchomekea mambo
hayo machafu lakini akishaona dalili kama hizo huwapotezea.