Wema Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye amekula kiapo cha kumchukia dada wa hiyari wa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’, Halim...
Wema Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye amekula kiapo cha kumchukia dada wa hiyari wa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’, Halima Kimwana ambaye wamekuwa na bifu kwa kipindi kirefu huku sababu zikiwa hazijulikani.
Wema Sepetu a.k.a Beautiful Onyinye.
Akipiga stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wema alisema ugomvi
wake na Halima Kimwana hautaisha na siku zote atamuonyesha chuki za wazi
sababu hana upendo naye hata kidogo.
Halima kimwana.
“Kusema kweli yule dada namchukia mpaka basi, simpendi na sitompenda
kamwe, haitatokea hata siku moja kwenye maisha yangu nikapatana naye,
yaani suala la kupatana mimi na yeye halipo kabisa, hata yeye mwenyewe
anajua simpendi maana damu zetu zimekataana, siwezi hata kuonyesha
upendo wa maigizo kwake,” alisema Wema.