MKALI wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade amesema yupo tayari kuja kumteketeza mkali wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena M...
MKALI wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade amesema yupo tayari kuja kumteketeza mkali wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
“Tanzania ni nchi nzuri najua na wanamuziki wake wapo vizuri, nimeambiwa kuna mwanamuziki anaitwa Shilole mwambieni tu nakuja kumteketeza na shoo zangu huwa hazina mpinzani.
“Nitafanya shoo ya mwaka ya kihistoria siku hiyo na lazima nimchukue Johnny wangu uwanjani hapo na kurudi naye kwetu Nigeria,” alisema Yemi.
Pia kutakuwa na burudani tofauti katika tamasha hilo ambazo ni ndondi, mechi kali kati ya timu ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar FC, Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na Wanamuziki wa Injili.