Kweli dunia ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe 'chafu', ...
Kweli dunia
ina mambo! Kuna watu wanajaribu kutumia kila fursa inayopatikana
kujinufaisha kwa kupata fedha hata ziwe 'chafu', kwao kitu cha maana ni
kupata utajiri kwanza.
Kundi la watu wanaofanya biashara ya
kusafirisha watu, wamekuwa wakitumia fursa ya ukosefu wa ajira kama
chambo cha kuwanasa vijana na kuwaingiza kwenye biashara haramu kama
ukahaba.
Hivi karibu kundi hilo linalosafirisha
watu lilipita katika vyuo vikuu kadhaa nchini Uganda na kuwaahidi
wanafunzi kuwa lingewatafutia kazi Ulaya na Marekani, kwani lina uzoefu
wa kutosha na kazi hiyo. Mmoja wa vijana 'waliobahatika' kupata nafasi
ya kwenda Ulaya kufanya kazi ni Sunday Bekunda (25), mwanafunzi wa mwaka
wa pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala.
Kwa bahati mbaya 'neema' ya kwenda
Ulaya iligeuka balaa baada ya kutekwa na kulazimishwa kufanya ngono na
wanawake mbalimbali huku akirekodiwa kwenye kamera za video.
"Ilikuwa ni Januari 2013, nilipokutana
na mwanaume mmoja anayeitwa Charles kutoka katikati ya Jiji la Kampala,
ambaye aliniahidi kunipeleka Kenya kufanya kazi katika kiwanda.
"Sikujua kuwa Charles alikuwa msafirisha watu. Alikuwa anaonekana kama mzazi wa makamo aliyefanya kazi kwa miaka mingi.
"Nilifungua moyo wangu na kumweleza
changamoto nyingi ninazopitia na namna nilivyo hangaika kutafuta kazi
ili nipate fedha za kulipia masomo ya ziada. Kwa kifupi ni kama nilikuwa
namwambia Charles kuwa sikuwa natafuta kazi bali nilikuwa nataka kazi
yoyote."
Safari ya Kenya
"Siku iliyofuata nilikuwa tayari kwa
safari na nilimkuta Charles akiwa kwenye gari la binafsi aina ya Toyota
Noah. Alikuwa pamoja na wasichana sita na wavulana wawili. Alituambia
kuwa tutaingia Kenya kwa kupitia mpaka usio rasmi unaoitwa Chepskunya.
"Tukiwa njiani, Charles alikuwa
anaongea sana na kutusisitizia kuwa 'tusimwangushe' tukifika huko.
"Tulipofika Kenya walituchukua na kutuingiza kwenye nyumba moja nzuri ya
makazi ya watu, hapo tulikutana na wenzetu 15, wavulana wawili kutoka
Rwanda na Wakenya 13."
Kutekwa
"Charles alituacha hapo tukiwa chini
ya mwanamke mmoja na wanaume wanne wenye miili iliyojengeka vyema. Watu
hao walianza kutupiga makofi na kutulazimisha tuvue nguo. Ndipo
nilipobaini kuwa kilichoonekana kama ni safari sasa imegeuka utekaji
"Baada ya kupigwa tuliambiwa tutoe
mifukoni kila kitu tulichokuwa nacho na kuweka juu ya meza. Nilishtushwa
nilipoona vyeti vya wanafunzi wa Uganda kutoka Vyuo Vikuu vya Kyambogo,
KIU (Kampala International University), Nkumba na UCU (Uganda Christian
University). Hata vyuo vya Kenya vilikuwapo.
"Mwanamke alitutishia kutuua kama
tusingetii walichosema. Kudhihirisha alichokuwa anamaanisha,
alituonyesha mkanda wa video wa mtu akiuawa na kupasuliwa tumbo.
"Halafu wakaweka video vyingine iliyotuonyesha biashara tutakayokuwa tunaifanya, ambayo ni kuigiza picha za ngono."
Ratiba ya kufanya ngono
"Walituongoza hadi ghorofa ya juu na
kutuweka katika vyumba tofauti. Katika chumba nilichokuwepo aliingia mtu
na kuniambia nitoe nguo kisha akanipa chupi tatu zinazobana.
"Hicho chumba kilikuwa na mwanga mkali
na kamera za CCTV katika kila kona. Baadaye wakamleta Bridget, mmoja wa
wasichana niliotoka nao Uganda, kisha wakaniambia kuwa nipo huru
kufanya naye ngono. Walipoondoka na kufunga mlango, Bridget alianza
kulia na kupiga kelele.
"Matukio mabaya yalianza rasmi siku
iliyofuata wakati yule mwanamke alipoingia kwenye chumba changu akiwa
ameshika mikanda mitatu ya ngono. Baadaye waliletwa wanawake na wanaume
niliokuja nao nikaambiwa nifanye nao ngono wakati watu wengine
wakirekodi kwa kutumia kamera kubwa.
"Nilipoishiwa nguvu, yule mwanamke
alitoka nje na kurudi halafu alinichoma sindano yenye dawa ambayo
ilinifanya nipate nguvu tena na kuendelea. Nikapewa ratiba ya kulala na
wanawake asubuhi, wavulana jioni (mashoga) na wanawake watu wenye umri
mkubwa usiku.
"Wanawake hao walikuwa wanawalipa wale
jamaa ili tufanye nao ngono. Kuna wakati nilikuwa nalazimishwa kulala
na wanawake saba kwa siku huku nikipata maumivu makali."
Mauaji
"Baada ya wiki tatu wote tuliitwa
sebuleni na kupewa taarifa kuwa mmoja wetu, aliyeitwa Sam Muteesi kutoka
Uganda, alikuwa amekataa kuwatii kwa hiyo alitakiwa auawe mbele yetu.
Walimfunga kwenye kiti, japokuwa alikuwa akiomba sana msamaha
walimfunika usoni kwa kutumia begi hadi alipokufa.
"Kwa kipindi chote cha Januari na
Februari 2013, nilikuwa nikifanya ngono za kila aina kila siku huku
nikitumia dawa za kulevya na pombe
"Mwanzoni mwa Machi, Charles alikuja
kwenye chumba changu na kuniambia kuwa ninatakiwa kwenda kuoa Uingereza.
Halafu akafungua kompyuta yake na kunionyesha picha ya mwanaume mzee
mzungu.
"Akaniambia nipite mbele ya kompyuta hiyo nikiwa nimevaa chupi nilizopewa ili huyo mzungu anione (kupitia Skype) kama nifaa.
"Huyo mzungu alinipenda, hivyo Charles
akawa amepata 'dili' ambayo ingenipeleka Uingereza, lakini kwa kuwa
sikuwa Mkenya nilitakiwa nirudi Uganda kuchukua hati ya kusafiria.
Atoroka
"Wakati tukivuka mpaka kuingia
Uganda, nilifanikiwa kukimbia pale
Mbale tulipokuwa tumesimama kunywa chai. Nilitoa taarifa yangu na
kufunguliwa faili namba SD REF 65/19/03/2013. Kwa kuwa Charles alikuwa
mtu mwenye nguvu (kifedha) hakufanywa chochote.
"Kutokana na mateso niliyopitia
nilikuwa kama kichaa, nililazwa katika Hospitali ya Vichaa ya Butabika
na nilipewa matibabu kati ya Agosti na Desemba 2013.
"Pia nilipimwa vipimo vingine na
kugundulika kuwa nilikuwa na maambukizi yote makubwa ya magonjwa ya
zinaa."Nimeamua kusimulia habari yangu kama sehemu ya kampeni ya
kuwaonya vijana wa vyuo vikuu kuwa makini na watu wanaowaahidi
kuwatafutia kazi nje ya nchi."
Imeandaliwa na Goodluck Eliona kwa Msaada wa Redio Netherlands Worldwide (RNW)