Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kuvamiwa na kundi l...
Siku chache baada ya msanii wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel kuvamiwa na
kundi la watu akiwa nyumbani kwa Wema Sepetu akitaka kuadabishwa kwa
madai ya kutembea na mume wa mtu, msanii huyo ameamua kumuandikia waraka
mwenye mume.
Aunt alifikia uamuzi wa kuandika waraka huo baada ya siku chache
baadaye tena kuandikwa habari juu ya kunaswa jijini Mwanza akiwa na
mnenguaji wa Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moze Iyobo ambaye ni mume wa
mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mwengi.
Waraka huo ambao unapatikana kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu:
“Dah! Kwa nini mimi kila siku, mimi kweli jamani hakuna wengine huko? Basi utashindwa hata kusalimiana na watu ktk hii dunia na yote ni wewe dada wa Mbagala, Mwengi.
“Dah! Kwa nini mimi kila siku, mimi kweli jamani hakuna wengine huko? Basi utashindwa hata kusalimiana na watu ktk hii dunia na yote ni wewe dada wa Mbagala, Mwengi.
Una nini lakini na mimi, unapita unaongea uongo wee nakunyamazia, sio
kama ni mpuuzi ila najitahidi kulinda kaheshima kangu hakahaka
kalikobaki hebu nenda ‘kadeal’ na wa dizain zako plz mimi sitaki Mwengi,
sitaki mm sio mnuka jasho mwenzio. Ni ngumu sana kuyapata unayoyataka.
Mume mume, tukilala mume, tukiamka mume, we unamjua mume wewe au! Dah
yaani ngoja niache tu mana naona ndio nazidi kuharibu …. still mimi ni
Mrs Demonte na itabaki kuwa hivyo forever.
Ukilizungumzia sakata lake na mke wa mtu huyo, Aunt alisema: “Huyu
mwanamke kuna kitu anatafuta, anataka kuniharibia heshima yangu lakini
hataweza, mimi ni Mrs Demonte tu.
“Si anasema mimi namchukulia mume wake, sasa ngoja nitaweka mtego,
nitamchukulia kwelikweli ili kama ni kukinukisha akinukishe kihalali.”