Inaonekana mashabiki wa Roma Mkatoliki hawajaafikiana na uamuzi wake wa kurekodi wimbo na Rais wa Masharobaro, B...
Inaonekana mashabiki wa Roma Mkatoliki hawajaafikiana na uamuzi wake wa kurekodi wimbo na Rais wa Masharobaro, Bob Junior.
Roma ameiambia Bongo5 kuwa kwa miaka saba amekuwa akifanya muziki
wake bila matatizo lakini kitendo cha kurekodi wimbo na Bob Junior
kimegeuka kero kwa wengine.
“Baada ya kusema nafanya kazi na Bob Junior kuna kitu ambacho
kimetengenezeka katika vichwa vya watu,” amesema Roma. “Kufanya kazi na
Bob Junior kumekuwa na matokeo mabaya eti ‘umefanya kazi na mpaka poda,
umefanya kazi na mkata viuno, umefanya muziki kwa miaka saba unafanya
muziki na mpaka lips stick, yaani na wewe unaanza kukata viuno;! Hawa
mashabiki wanachanganya wakati wao ndo wanasema ‘Roma kila siku unaimba
kitu kile kile unatakiwa ubadilishe hata ladha’. Kwahiyo watu wameanza
kuikataa nyimbo kabla hata hawajaiona. Mimi naona kinachotakiwa ni
kuwaelimisha kwa sababu wengi wao hawafuatilii muziki na hawaulewi
ambapo nimetokana ndio maana nikawapa mfano Kalapina alishawahi kuimba
na Q Chillah na ngoma ikafanya vizuri sisi ni wasanii kushirikiana na
kufanya muziki ni sehemu ya maisha yetu.”