Rapper kutoka Morogoro Afande Sele amesema leo ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya mwanae Tunda, anapata mtihani wa kwanza wa kusherehekea sik...
Rapper kutoka Morogoro Afande Sele amesema leo ikiwa ni siku ya
kuzaliwa ya mwanae Tunda, anapata mtihani wa kwanza wa kusherehekea
siku hiyo wakati mama yake hayupo tena duniani.
Akizungumza leo ,Afande Sele amesema ingawa alikuwa na
matatizo na mke wake wakati yupo hai lakini bado alikuwa ni kiungo
kibubwa kwenye familia yake.
“Leo ni birthday ya mwanangu Tunda, leo katimiza miaka 13 nataka
niende shule kumsalimia lakini ni birthday ya kwanza bila mama yake,”
amesema Afande.
“Napata wakati mgumu sana hata kusema siwezi kwa sababu siku zote
mzazi mwenzangu alikuwa mtu ambaye anafanya kazi kubwa, matatizo ya
kawaida yapo mpaka anaondoka duniani hatuko sawa lakini masuala ya
watoto alikuwa yupo mbele sana kusema ukweli
Alikuwa anajali sana watoto wake, anafuatilia hatua moja hadi nyingine, kipindi hiki ambacho nipo peke yangu yeye hayupo najikuta kwamba navaa kofia ambayo sikutegemea. Nimeona kwamba uzito wa tukio la kuondoka kwake ni mkubwa kuliko nilivyokuwa nikifikiria mwanzoni.”
Alikuwa anajali sana watoto wake, anafuatilia hatua moja hadi nyingine, kipindi hiki ambacho nipo peke yangu yeye hayupo najikuta kwamba navaa kofia ambayo sikutegemea. Nimeona kwamba uzito wa tukio la kuondoka kwake ni mkubwa kuliko nilivyokuwa nikifikiria mwanzoni.”
“Leo nilikuwa nina kazi nifanye Chalinze na mpaka sasa kazi hiyo
ninayo lakini siwezi kwenda kwenye kazi moja kwa moja bila kwenda
kumuona mtoto shuleni kwa sababu alizoea siku kama ya leo mama yake
ataenda mapema sana, baba asipomuona anajua yupo mtaani anatafuta maisha
yetu lakini mama yupo mjini. Sasa leo hii mama yake hayupo, nakuwa
mimi ndio baba ndio mama, na ndio kila kitu kwahiyo najikuta na wakati
mgumu sana kuona kwamba katika mwezi ambao nimempoteza mama mtu na ndo
mwezi ambao mtoto wangu alizaliwa, leo ni birthday ya mwanangu Tunda,
napata wakati mgumu sana na mama yake hayupo,” amesema Afande.
Mama Tunda alifariki dunia usiku wa August 14 mkoani Morogoro na kuzikwa katika makaburi ya Kolla yaliyopo mkoani humo.