Archive Pages Design$type=blogging

KWELI JACK PATRICK NI MPENZI WANGU - JUX

MALOVEE! Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na ...

MALOVEE! Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Staa wa Bongo Fleva anayetamba na wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’.
Jux ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva, alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti Fiesta 2014.
Akijibu swali la mwandishi wetu lililomtaka afungukie penzi lake na Jack ambalo alikuwa akichengachenga kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya habari, Jux alianza kwa kukiri kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na walidumu kwa takriban miezi saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya kulevya.
Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’.
Alisema tangu aanze kuyajua mapenzi, Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake ingawa wakati anapatwa matatizo walikuwa wametibuana kwa kipindi cha wiki mbili.
“Nilisikitika sana niliposikia amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama anafanya hiyo biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua yupo Bongo na nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.
Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema hana taarifa hizo.“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
Jux akiwa na Jack Patrick.
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.

COMMENTS

Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: KWELI JACK PATRICK NI MPENZI WANGU - JUX
KWELI JACK PATRICK NI MPENZI WANGU - JUX
http://api.ning.com:80/files/Qvoxp7jhEtKU*Mzne4V3ndD5ZAzRfzU6P1HGo0RgYqk9Vej7zYaN-p*Th9sf9RusK*IruvxVLuSjlzYJlmpmRpUszjhpKzAv/jux.jpg
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/kweli-jack-patrick-ni-mpenzi-wangu-jux.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/08/kweli-jack-patrick-ni-mpenzi-wangu-jux.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago