Kama wewe ni jaji unayetumia vithibitisho vya unachokiona kwa macho peke yake, basi ukitakiwa kutoa hukumu kwa kinachoonekana kwenye pic...
Kama wewe ni jaji unayetumia vithibitisho vya unachokiona kwa
macho peke yake, basi ukitakiwa kutoa hukumu kwa kinachoonekana kwenye
picha hizi za Nicki Minaj na Drake lazima utasema ni zaidi ya
marafiki,sio? Japo wao walishawahi kuzungumza na kusema ni kaka na dada
licha ya ukaribu ambao wameonekana kuwa nao.
Nicki Minaj ameendelea kupromote video ya ngoma yake mpya ‘Anaconda’
ambayo aliiachia audio siku chache zilizopita. Kupitia Instagram yake
Minaj ameshare picha zingine akiwa anampa ‘lap dance’ rapper Drake
ambaye ataonekana kwenye video hiyo inayotarajiwa kutoka kesho Jumatano
(Agosti 20).
Nicki Minaj pia atatumbuiza single hiyo ‘Anaconda’ katika tuzo za MTV VMA za mwaka huu zitakazofanyika Jumapili hii.
