Muimbaji anayefanya vizuri ...
Muimbaji anayefanya vizuri na wimbo wa Serebuka, Mwasiti
ameshangazwa na watu wanaomzushia kuwa ni mjamzito na kukanusha japo
amedai anatamani kuwa na mtoto.
Akizungumza leo, Mwasiti amesema hana mpango wa kuolewa kwa
sasa na wala hana ujauzito kama watu wanavyozusha. “Nasikia eti watu
waniambia nina mimba, sina mimi na sijui hizo habari watu wanazipata
wapi,” amesema. “Sina mpango wa kuolewa, vyote watu wanazusha tu. Kweli
hakuna mwanamke asiyetamani kuwa na mtoto hata mimi napenda sema ni
majaliwa, mambo yote anapanga Mungu,” ameongeza.
Katika hatua nyingine Mwasiti amezungumzia ujio wa wimbo yake mpya uitwao ‘Leo’ aliomshirikisha Godzilla.
“Nina ngoma mbili ambazo ninategemea ziende mtaani. Nina Leo ambayo
nimemshirikisha Godzilla halafu nina Kisigino ambayo nimeimba mimi peke
yangu lakini sijajua itatoka ipi, Nyimbo zote mbili ni aina mbili
tofauti za muziki. Muziki wa Mwasiti wa sasa hivi upo kwelI leo, lakini
kwenye Leo tumeimba tofauti, mtashangaa kumuona Godzilla ambaye
amebadilika sio Godzilla ambaye amezoeleka, ni Godzilla mwingine kabisa,
nimeamua kumbadilisha.”
“Kwahiyo ukisikiliza Leo utasikiliza ladha mbili tofauti, utamsikia
Godzilla na Mwasiti. Hiyo tumefanya chini ya producer Chizan Brain, B
Records na Kisigino ni wimbo wa kuchezeka na tumefanya na Shebby
Records. Kwahiyo yoyote kati ya hizo inaweza ikatoka lakini itaanza
video kwanza.”