Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic. KAZI! Hivi ndivyo utakavyosema msimu h...
KAZI! Hivi
ndivyo utakavyosema msimu huu wa Ligi Kuu Bara kutokana na Kocha Mkuu wa
Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic kutumia mbinu zinazotumiwa na
Mbrazili, Marcio Maximo.
Maximo, tangu atue Yanga, ameonekana akitumia mbinu tatu kuwafundisha
wachezaji wake katika kuhakikisha timu yake inapata matokeo mazuri
ikiwemo kutwaa ubingwa.
Moja ya mbinu anazozitumia ni kuwatumia mawinga na mabeki katika
kushambulia lango la timu pinzani kwa kutumia mipira ya krosi na kona.
Pia kufunga mabao kwa kupiga mashuti ya mita 20 kwenye goli la timu
pinzani na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ‘counter attacks’.
Katika mazoezi ya hivi karibuni ya Simba yanayoendelea kwenye Uwanja wa Ununio, Boko jijini Dar es Salaam, Logarusic alionekana kutumia mbinu hizo tatu anazozitumia Maximo.
Katika mazoezi ya hivi karibuni ya Simba yanayoendelea kwenye Uwanja wa Ununio, Boko jijini Dar es Salaam, Logarusic alionekana kutumia mbinu hizo tatu anazozitumia Maximo.
Wakati anaendelea na mazoezi hayo, Logarusic alionekana kuwapa
maelekezo hayo kwa kuwataka kabla ya kupiga krosi kuangalia wachezaji
wenzao watakaofikiwa.
Mcroatia huyo alionekana akiwapa maelekezo zaidi viungo washambuliaji
Uhuru Selemani, Awadhi Juma, Said Ndemla na Shaban Kisiga kupiga krosi
hizo.
Zoezi hilo la kupiga krosi liliwajumuisha mabeki wa pembeni wa timu
hiyo, Said Nassor ‘Chollo’, Issa Rashidi ‘Baba Ubaya’ na beki mpya
kutoka Kagera Sugar, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.
Kocha huyo, alionekana kuwa mkali na kuwafokea wachezaji hao pale walipofanya kinyume na maelekezo.
Kocha huyo, alionekana kuwa mkali na kuwafokea wachezaji hao pale walipofanya kinyume na maelekezo.
Hiyo ni dalili tosha kwamba, msimu ujao ushindani utakuwa mkubwa zaidi, hasa Simba na Yanga zitakapokutana.