Manager wa Tip Top Connection na Diamond Platnumz Babu Tale inasemekana anamsimamia kwa sasa Shilole kama msanii wake kwa kile a...
Manager
wa Tip Top Connection na Diamond Platnumz Babu Tale inasemekana
anamsimamia kwa sasa Shilole kama msanii wake kwa kile ambacho
kimeelezwa na Soudy Brown kuwa deni alilokua anadaiwa Shilole.
Deni ambalo linasemwa kuwa Babu Tale alilipa ni la gari ambalo alikua
akidaiwa Shilole hivyo wakakubaliana kuwa watakua wakikatana kwenye
show tofauti mpaka deni hilo litakapoisha.
Soudy Brown kaongea na Shilole ambaye kasema ‘Mbona mimi sijui hayo
mambo,sio kweli huo uwongo watu waongo sio kweli,gari ni langu na nina
kila kitu changu watu wana donge kuona mimi Shilole naendesha Toyota
Harrier Lexus nilinunua Milion 24′
‘Babu Tale ni mtu anayenisaidia kwenye kazi zangu na namheshimu kama
kaka yangu nimeanza nae kazi mwaka huu na sina mkataba nae’.