Baada ya kuwepo na tetesi za b...
Baada ya kuwepo na tetesi za beef kati ya rapper wa kike mzaliwa
wa Australia Iggy Azalea na Nicki Minaj, marapper hao Jumapili
iliyopita (Agosti 24) walikutana backstage kwenye tuzo za MTV VMA na
kuziuwa kabisa tetesi hizo.
Baada ya Nicki kuperform single yake mpya ‘Anaconda’ akiwa anajiandaa
kuhojiwa na MTV backstage ndipo Iggy alipita na kumpongeza kwa
kumwambia “You did great,” , na Nicki akamjibu “Thank you honey,” huku
akiwa na tabasamu kubwa usoni.
Hisia za kuwepo kwa beef kati ya Nicki na Iggy zilikua zaidi baada ya
kauli aliyoitoa Nicki wakati wa tuzo za BET, ambayo baadae alikuja na
kujitetea kuwa vyombo vya habari vilimuwekea maneno mdomoni.
Hata hivyo Nicki Minaj pia aliwahi kumpongeza Iggy Azalea hadharani kwa mafanikio ya single yake ya ‘Fancy’.