Wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake leo wanatarajiwa kushuhudia tamasha la Kili Music Tour litakalofanyika uwanja wa Jamhuri. Muonek...
Wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake leo wanatarajiwa kushuhudia tamasha la Kili Music Tour litakalofanyika uwanja wa Jamhuri.
Muonekano wa jukwaa litakalotumiwa na wasanii katika uwanja wa Jamhuri
Tamasha hilo ambalo mpaka sasa limezunguka mikoa 6 litawakutanisha
wasanii zaidi ya 10 katika jukwaa moja waliofanya vizuri katika muziki
kwa kwa kipindi cha 2013/2014.
Wasanii hao waliowasili Dodoma siku ya jana wamesema wamejipanga
kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Dodoma wanapata burudani ambayo miko
mingine imeishuhudia.
Akihojiwa na kituo cha Dodoma FM, Ben Pol ambaye alianzia muziki
mkoani hapo amesema siku zote anajisikia fahari kutoa burudani mbele ya
mashabiki wa nyumbani na kuelezea namna wasanii wengine walivyo na ari
ya show hiyo.
Wasanii wengine wanaotarajiwa kupanda jukwaani ni Khadija Kopa,
Mwasiti, Shilole, Rich Mvoko, Christian Bella, MwanaFA, Izzo Bizness,
Joh Makini, Nikki wa Pili na Gnako Warawara.