Rapper Darassa amemshauri mwenzie Roma Mkatoliki kuwa serious hata ikibidi kukata mauno kwenye video ya wimbo ‘Maumivu’ aliofanya na Bob...
Rapper Darassa amemshauri mwenzie Roma Mkatoliki kuwa serious
hata ikibidi kukata mauno kwenye video ya wimbo ‘Maumivu’ aliofanya na
Bob Junior.
“Mimi napenda muziki wa aina yoyote na ninaweza kusikiliza muziki wa
Bob Junior nikiupenda sina tatizo, napenda muziki mzuri,” Darassa
amekiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV. “Kwenye video nitapenda
sana kama Roma akahakikisha Bob Junior hamzidi kwenye viuno, yaani
nitapenda sana kama Roma atakuwa serious, ahakikishe analeta changes
kwenye hii tasnia.”
Unadhani Darassa alikuwa serious alikuwa ni utani kwa Roma?