Mwanamke huyo akiwa na boksi, huku akila wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo (Pembeni ...
MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika,
amewashangaza wapita njia baada ya kuonekana akitembea huku akipiga
kelele katika mitaa ya Kariakoo.
Mwanamke huyo aliyekuwa amebeba boksi huku juu yake kukiwa na samaki
wadogo wadogo, kitunguu, kipande cha chungwa na vinginevyo, aligeuka
kituko baada ya kelele zake kuwashangaza wapita njia waliokuwa
wakimuangalia na wengine wakimpisha njia kwa kumhofia. Hata hivyo,
haikufahamika mara moja tatizo la mwanamke huyo.