Thomas Ulimwengu. Washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP M...
Washambuliaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wa klabu ya TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wanawasili nchini
keshokutwa alfajiri (Julai 16 mwaka huu) kwa ajili ya mechi dhidi ya
Msumbiji (Mambas).
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika (AFCON)
kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Mambas itachezwa Jumapili (Julai 20
mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ulimwengu na Samata watawasili saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir
wakitokea Tunisia ambapo timu yao ya TP Mazembe imepiga kambi kwa ajili
ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi
Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na
mwamuzi Mahmoud Ashour kutoka Misri.
Stars itarejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa (Julai 18 mwaka
huu) kwa ajili ya mechi hiyo wakati Mambas nao wanatarajiwa kutua siku
hiyo hiyo. Mechi ya marudiano itachezwa kati ya Agosti 1 na 3 mwaka huu
nchini Msumbiji.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)