Msanii wa muziki na mmiliki wa Ray foundation, Rehema Chalamila aka Ray C amefunguka kwa kusema kuwa alhamisi (july 10) alivamiwa na ku...
Msanii wa muziki na mmiliki wa Ray foundation, Rehema Chalamila
aka Ray C amefunguka kwa kusema kuwa alhamisi (july 10) alivamiwa na
kupigwa na msanii Chid Benz.
Akizungumza leo ,Ray C amesema kuwa Chid Benz anatafutwa na polisi baada ya kufanya tukio hilo.
“kweli alinivamia alhamisi usiku, amenipiga mimi na amefanya
uharibifu wa mali, mimi nashangaa usiku navamiwa ata sikujua nani
amemuonyesha nyumbani kwangu, mimi nilikuwa namtafuta kwa sababu ya show
ya kuelimisha vijana na maswala ya madawa ya kulevya, yeye
akalichukulia kivingine kabisa, nahisi amechanganyikiwa na madawa ya
kulevya, kweli itakuwa amechanganyikiwa na madawa, hayuko sawa kabisa.
Sasa hivi nina RB yake , kwaiyo anatafutwa na polisi, kokote atakapo
kamatwa anawekwa ndani, najua atajifisha lakini ipo siku atakamatwa na
polisi tu. Watanzania wanatakiwa kushirikia na polisi ili akamatwe kwa
sasabu Chid hayuko sawa kabisa” Alisema Ray C.