Msanii wa muziki, Ali Kiba amefunguka kwa kusema kuwa anapenda kufanya kollabo na wasanii wachanga ili kuwasaidia kimuziki kwa sababu ...
Msanii wa muziki, Ali Kiba amefunguka kwa kusema kuwa anapenda
kufanya kollabo na wasanii wachanga ili kuwasaidia kimuziki kwa sababu
yeye mwenyewe alipata shida sana kutoka kimuziki.

Akizungumza na 255 ya XXL ndani ya Clouds Fm, Ali kiba alisema
wakati anataka kutoka kimuziki alitamani kutafuta wasanii wakubwa wa
kufanyanao kollabo lakini alishindwa.
“Napenda kuwasaidia kutokana na mimi mwenyewe nilipata tabu sana,
nilitamani kufanya ngoma na mastaa, lakini kwa bahati nzuri haikutokea,
Dully aliweza kufanya nyimbo na mimi kwa mapenzi yake, alinisikia kwa
sababu tulikuwa tunakaa opposite, aliweza kusikia bets akaingia moja kwa
moja mpaka ndani ,nadhani unamjua Dully mambo yake ya utundu,
akaniambia wewe kumbe ni msanii, nikamwambia yeah mimi naimba,
akaniambia sawa basi, umefanya wapi?, niikamwambia, kwaiyo akajua mimi
nishaendaga mpaka studio, alikuja pale akaamini na mimi nikaimba
nilifuraisha sana kwakweli, akasema twende tukafanye , akajaza mafuta
gari yake ,yeye mwenyewe kwa pesa yake, sikufichi nasumbuliwa sana,
nasumbuliwa sana kwa kollabo , mpaka nikisema hivi anaona kama
hawanielewi , lakini mimi nishajua umuhimu wangu ni kuwasaidia , kwaiyo
nawasaidia wasanii wachanga kutokana na mateso ambayo nimepata , kwaiyo
napenda kuwatoa kama unavyowaona akina Ommy Dimpoz na wengine wengi”
Alisema Ali Kiba