Muongozaji mkongwe wa filamu nchini, George Tyson leo ametimia 40 toka afariki dunia May 31 kutokana na ajali ya gari maeneo ya Gairo, M...
Muongozaji mkongwe wa filamu nchini, George Tyson leo ametimia
40 toka afariki dunia May 31 kutokana na ajali ya gari maeneo ya Gairo,
Morogoro akitokea mkoani Dodoma, ambapo aliyekuwa mke wake Monalisa
amemtumia ujumbe.
Monalisa akiwa na marehemu Goerge Tyson enzi za uhai wake pamoja na mtoto wao
Kupitia Instagram Monalisa ameandika: George,40 days toka
ulipoondoka..mengi yametokea mmh! I wish ungefumbua macho dakika tu
uone, unakumbuka ile story ulinihadithia ulitaka kuiandika tuifanye
movie ukaipa jina la ‘When I come back ‘ yaani kama ulijitabiria,
mwanzoni nilikuwa nadhani ni sinema unatuchezea lakini nimeamini You are
no longer with us, But ur Angel is smiling now,wala usiwe na hofu we
know upo kwenye mikono salama, tunakuombea na maisha yetu yanaendelea
najua hicho ndicho kitu ungependa kukiona kwetu ingawaje juzi tuliitwa
na @tv1tanzania nilipofika pale nikashindwa kujizuia, tutakukumbuka
daima @jojityson”
Baada ya kifo chake mwili wake ulisafirishwa hadi Dar es salaam
kwaajili ya kumuaga na baada ya hapo mwili ulisafirishwa kwenda kwao
Kenya kwa mazishi.