Alama ya verified ndio inatambulisha ukurasa halali wa mtumiaji kwenye mitandao mingi sana. Alama hii ni muhimu sana hasa kwa...
Alama
ya verified ndio inatambulisha ukurasa halali wa mtumiaji kwenye
mitandao mingi sana. Alama hii ni muhimu sana hasa kwa watu maarufu
wanaotumia mitandao ili kuepuka kuwepo kwa kurasa feki ambazo
haziwahusu.
Hivi sasa mtu maarufu ambaye page yake ya facebook imekuwa verified
ni mchezaji wa kikapu kwenye timu ya Oklahoma City Thunders “Hasheem
Thabeet”. Ukurasa wake wa twitter ulikuwa verified siku nyingi na hivi
sasa mashabiki wake wa facebook watakuwa na uhakika kwasababu na
facebook wame-verify ukurasa wake.