Wanajeshi wa kupambana na ugaidi nchini Kenya (ATPU) wanawashikilia raia watatu wa Tanzania waliokamatwa wakijaribu kuvuka mpaka wa Soma...
Kamanda wa Polisi Lamu Mashariki amethibitisha kukamatwa kwa watatu
hawa ambao wote wana umri chini ya miaka 22 ambao kwa sasa wanashikiliwa
na maafisa wa kupambana na Magaidi Kiunga mpaka wa Kenya na Somalia
ambapo baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa Mahakamani.
Kukamatwa kwa watatu hawa kunafikisha idadi ya vijana sita wa
Kitanzania waliokamatwa nchini Kenya ambao wanatuhumiwa kujiunga na
mtandao wa kigaidi ambapo wengine watatu wanashikiliwa kwenye gereza la
Kamiti waliokamatwa Kiamboni.
Miongoni mwao ni Bakari na Daudi ambapo walipohojiwa wamesema >>> ‘Tumeambiwa
kwamba Somalia kuna Waislamu na wako katika hali ngumu, kuna majeshi
mengi yanawanyanyasa Waislamu kwa hiyo kama Muislamu inabidi uende kutoa
support kwa ndugu zako, kutokana na imani yangu kujengeka katika dini
ndio nikajikuta naunga safari’
Haya yanajiri baada ya vijana kadhaa wa Kenya kukamatwa mpakani
walipokua wakifanya mpango kuvuka mpaka na kuingia Somalia vilevile
msajili wa kundi la Al Shabaab amekamatwa akiwapeleka vijana wawili wa
Mombasa kwenda kujiunga na Al Shabaab mjini Garisa.
Wakati huohuo Polisi wanawasaka vijana waliotumwa na Al Shabaab
kwenye mataifa ya Kenya na Tanzania kusubiri kupewa maagizo ya kundi
hilo kutekeleza mashambulizi.
Unaweza kuwasikiliza wakiongea hapa chini.