Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye aliwahi kuhisi au kutegemea kama Marehemu Adam Kuambiana ambaye alikua muongozaji[Director] wa ...
Ni
kitu ambacho hakuna mtu ambaye aliwahi kuhisi au kutegemea kama
Marehemu Adam Kuambiana ambaye alikua muongozaji[Director] wa filamu
nyingi za Kitanzania kumbe nae kashiriki kwenye video ya Mdogo Mdogo.
Adam Kuambiana ambaye alifariki May 17 2014 wakati akiwa kambini kwa
ajili ya filamu yake mpya ametajwa na Diamond kuhusika na utengenezaji
wa Script[muongozo] wa video ya Mdogo Mdogo iliyotengenezwa South Africa
na God Father.
‘Baby alinambia ni mzuri sana nikamfata nikamwambia nina nyimbo yangu
nataka uniandikie stori wimbo wangu unaenda hivi na hivi akanambia ni
vizuri nikifika studio niisikilize kwanza huo wimbo’
‘Nikawa nae studio nakumbuka nilikuwa nae studio kwa Tudd Thomas pale
THT akawa anasikiliza wimbo akawa ananambia namna stori inavyotakiwa
kwenda so naweza kusema stori inavyoanza picha hata ya kupata Stori ni
Kuambiana ndiye aliyenipa.
Bonyeza play kumsikiliza Diamond.