Davido ni mtu ambaye huwa anaonyesha vitu vingi anavyonunua kama baadhi ya mastaa lakini kwa upande wa Davido vinahusika vitu...
Davido ni mtu ambaye huwa anaonyesha vitu vingi anavyonunua kama
baadhi ya mastaa lakini kwa upande wa Davido vinahusika vitu vya gharama
sana. Ukicheki utaona post akionyesha saa za Rolex ambazo zina material
ya dhahabu, magari ya kifahari,nyumba na vitu vingine.
Baada ya kuulizwa kuhusu ishu hii ya kupenda kuonyesha mali zake
kwenye instagram Davido alijibu,”Sitaweza kuita kama ni kujionyesha kwa
mali zangu. Yale ni magari yangu,zile pesa zangu na pia ile ni page
yangu.
Sio lazima uni follow kwenye instagram wala kunifata kwenye mtandao
wowote wa kijamii. Ingekuwa tofauti sana kama nataka kujitangazia mali
zangu basi ningetumia mabango ya barabarani lakini sifanyi hivyo”