Diamond Platinumz hivi anaendelea kupambana kuupeleka muziki wa Tanzania katika level ya kimataifa na hivi sasa amepanga kuchia video mb...
Diamond Platinumz hivi anaendelea kupambana kuupeleka muziki wa
Tanzania katika level ya kimataifa na hivi sasa amepanga kuchia video
mbili kwa mpigo.
Bila
shaka video hizo ni moja aliyofanya na Iyanya Uingereza ambayo amepanga
iwe kwa ajili ya mashabiki wa ndani na nje ya nchi na nyingine ya asili
‘MdogoMdogo’ ya Tanzania ambayo mimi naamini pia itafika mbali.
Hata hivyo Diamond ana ombi kwako wewe shabiki wake na ameandika
katika ukurasa wake wa Facebook, saidia katika hili tupate tarehe rasmi
ya kuzipokea video mbili kwa mpigo.
“Nataka Kudondosha video Mbili kwa Mpigo… tafadhari niambie, lini niziachie…???
[ I wanna drop 2 videos at da same time... Now you tell me, when should I let them out...??]”
Diamond ameweka baadhi ya picha zinazokuwa kwenye video yake akiwa kazini kama muigizaji fulani.