Msanii wa muziki Nasib Abdul aka Diamond Platinum amesema kuwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za BET nchini Marekani kimempa ...
Msanii wa muziki Nasib Abdul aka Diamond Platinum amesema kuwa
kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za BET nchini Marekani kimempa
connection nyinyi za kimuziki pamoja na kollabo ambazo zinaweza
zikasaidia zaidi.
Akizungumza na waandishi jijini Dar es salaam jana baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K Nyerere akitokea
Marekani, Diamond alisema amepata connention nyingi ambazo kwa sasa ni
mapema kuziweka wazi.
“Kiukweli nyingi sana, ata wakati nipo njiani nilikuwa naongea na
manager kidogo , lakini siyo vizuri kuanza kuvisema sasa hivi, naogopa
kivisema sasa hivi kwa sababu uongozi unajua, lakini kiukweli ni vitu
vizuri sana, ambavyo ata baadae vikitangazwa watu watafurahi, wataona
kweli tunafanya vitu, cha kwanza kabisa muhimu ukiacha kuuza muziki,
kollabo ni kitu ambacho kinasaidia , unajua kufanya kollabo na watu wa
nje kama tulivyofanya kollabo huku Tanzania, na ikafanya vizuri na
ikatupenyesha vizuri Afrika, tukifanya na mtu wa kule ( Marekani)
tunaingia kule kiurahisi” Alisema Diamond