Wacheza filamu maarufu kutoka nchini Marekani ambao pia ni wapenzi Angelina Jolie na Brad Pitt wanatarajia kurejea wakiwa pamoja kweny...
Wacheza filamu maarufu kutoka nchini Marekani ambao pia ni wapenzi
Angelina Jolie na Brad Pitt wanatarajia kurejea wakiwa pamoja kwenye
majumba ya sinema kwa kucheza filamu ya pamoja iliyopewa jina la “By The
Sea.” ambapo Angelina anatarajia kuongoza filamu hiyo huku wote wawili
wakiwa ndio watayarishaji.
Picha za filamu hiyo zitapigwa katika visiwa vya Malta na Gozo.
Jolie
amethibitisha habari hizo akisema kuwa anafurahi sana kuendeleza
mahusiano yake na kampuni kubwa ya utengenezaji filamu ya Universal
wakati akiwa anamalizia kutengeneza filamu ya ‘Unbroken’ na kuanza
kutengeneza filamu ya ‘By the Sea.
Kama wewe ni mpenzi wa filamu za Angelina Jolie tarajia mambo makubwa kutoka kwenye filamu hizo.