Stori: Chande Abdallah na Denis Mtima UNYAMA ulioje? Mtoto Fatuma Hassan (9) ...
Stori: Chande Abdallah na Denis Mtima
UNYAMA ulioje? Mtoto Fatuma Hassan (9) ambaye ni
mwanafunzi wa Shule ya Msingi Hekima iliyopo Tandale, Dar anadaiwa
kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha kuchomwa moto na mama yake mkubwa
aliyetajwa kwa jina moja la Diana (38), mkazi wa maeneo hayo, kisa
kikielezwa kuwa ni shilingi mia tano.
Tukio hilo lilitokea Juni 10, mwaka huu katika maeneo hayo ya Tandale
Sokoni ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mtoto wa mdogo wake kwa kile
kilichodaiwa kuwa alimchukua kwa ahadi ya kumsomesha lakini kuna madai
kuwa badala ya kufanya hivyo, alimnyanyasa.
Taarifa zilidai kwamba mama huyo aliamua kumfanyia ukatili mtoto huyo
akidai kuwa alichukua fedha hizo akiwa na mwanaye wa kumzaa kwa ajili
ya kwenda kutumia kununulia sambusa na juisi shuleni.
Ilisemekana kwamba kitendo hicho kilimkera mama huyo na kuamua kuwasubiri warudi ili awaulize kama kweli walichukua fedha hizo ambapo walikiri kuzitumia shuleni.
Ilisemekana kwamba kitendo hicho kilimkera mama huyo na kuamua kuwasubiri warudi ili awaulize kama kweli walichukua fedha hizo ambapo walikiri kuzitumia shuleni.
Wakizungumza na wanahabari wetu, majirani wa eneo hilo walisema kuwa
walimuona mtoto Fatuma akipigwa na mama’ke huyo mkubwa fimbo na kumchoma
moto mikononi pasipo kumpeleka hospitali huku akimpa onyo kali na
kumfungia ndani.
Walisema kuwa mwanamke huyo amekuwa akimfungia ndani na kwenda kwenye genge lake.
Mjumbe wa eneo hilo, Said Sundi na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pakacha, Ally Mdee wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mjumbe wa eneo hilo, Said Sundi na Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Pakacha, Ally Mdee wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wananchi walifikia hatua ya kufananisha tukio hilo na lile la mtoto
aliyefungiwa kwenye boksi mkoani Morogoro, Nasra Mvungi (marehemu),
walimkamata na kupiga simu katika Kituo cha Polisi cha Magomeni ambapo
askari walifika na kumchukua mwanamke huyo.
Pia walimpeleka mtoto Fatma kwenye Hospitali ya Magomeni anakopatiwa
matibabu huku mwanamke huyo akishikiliwa na polisi kwa ajili ya
mahojiano na alifunguliwa kesi ya kujeruhi yenye jalada namba
MAG/RB/5676/2014.