Majeraha aliyonayo kichwani Melina Mathayo baada ya kupigwa na bosi wake. ...
Majeraha aliyonayo kichwani Melina Mathayo baada ya kupigwa na bosi wake.
HAUSIGELI aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15,
ameumizwa vibaya sehemu za kichwani na kulazwa katika Hospitali ya
Mwananyamala jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na bosi wake aitwaye
Yasintha Rwechungura mkazi wa Boko.
Akiongea na mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina
amesema amekuwa akipigwa na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia
waya, brenda na vifaa vingine japo alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo hivi vya ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku
chache baada ya hausigeli aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi
wake aitwaye Amina Maige aliyepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti huyo aliyeletwa Mwananyamala leo alfajiri akiwa na hali mbaya
amefanya kazi kwa miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani
Kagera.
Melina alikuwa akiongea na mwanahanbari wetu akiwa na mpira wa
kuongezewa damu mwilini na amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa
matibabu zaidi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea tukio hilo