...

Afisa
habari wa Yanga sc, Baraka Kizuguto (kushoto) akiwa na Coutinho (kulia)
baada ya kuwasili nchini jana akitokea kwao nchini Brazil.
YANGA SC imemsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Andrey Marcel Ferreira Coutinho.
Mchezaji
huyo aliwasili jana mchana jijini Dar es salaam akitokea kwao nchini
Brazil tayari kwa kuanza kazi ya kuitumikia Yanga katika msimu wa
2014/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Coutinho aliwaeleza waandishi wa habari kuwa anajisikia furaha kuwa Tanzania, nchi ambayo watu wake wanapenda mpira.
Mchezaji
huyo haijui Tanzania, lakini ameifahamu kutokana na bosi wake Marcio
Maximo ambaye amechangia kwa asilimia zote kumleta nchini.
Bila
shaka wakati wanaongea na Maximo juu ya kuja kufanya kazi Tanzania,
Coutinho alihoji mambo mengi na mazingira ya Tanzania na kupewa majibu
na Maximo ambaye unaweza kusema ni mwenyeji wake.
Maximo
anafahamu utamaduni wa mashabiki wa Tanzania na alimweleza ukweli kiungo
huyo na yeye kuiamini Tanzania mpaka kusema anafurahia kufanya kazi
kwenye ardhi ya nchi hii ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Brazil kuna wachezaji wengi na vipaji vingi vya soka. Hii ni nchi inayosemekana kunukia mpira kila kona.
Tunaona wabrazil wengi wanafanya makubwa katika soka la sasa duniani, lakini miaka ya nyuma walitokea wachezaji wakali pia.
Unamkumbuka
Pele? Huko mbali, miaka ya karibuni tu, akina Ronaldo, Ronaldinho,
Ricardo Kaka`, Robinho, na sasa Neymar wametikisa soka la dunia.
Hawa ni
mfano tu, ukiamua kuwataja wachezaji wa Brazil waliofanya kazi nzuri
utaandika kwa muda mrefu na huwezi kumaliza, lakini ninachojaribu
kusema ni kwamba, Brazil ni nchi yenye vipaji vingi vya soka.
Kwa
wale waliobahatika kufika Brazil, wanajua wazi kuhusu hilo. Ukipita
mitaa mingi ya nchi hii, lazima uwakute vijana wanacheza soka.
Katika
maelezo ya Coutinho alisema amewahi kucheza barani Asia na alipata
uzoefu mzuri, hivyo anaamini chini ya makocha aliowazoea ataisaidia
Yanga.
Kucheza Asia sio jambo jepesi, huko pia kuna mpira na watu wana mipango mizuri. chanzo BARAKA MPENJA