Wakati wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lu...

Wakati
wanawake wengine wakionekana kubembeleza penzi na kujinyenyekeza
kwa wapenzi wao ili wasiachike, Lulu Michael anasema hana muda
huo kwani uzuri wake unatosha kuwavuta wanaume wa kila aina
kutoka katika kila kona ya Tanzania.....
Lulu
amedai kuwa inawezekana mwanaume wa kwanza kwake ndo chaguo
lake namba moja, lakini suala la kuanza kulilia mapenzi au
kuumia halipo na kamwe hawezi kufanya hivyo.
"Mapenzi
ni magumu hasa kwetu sisi wasanii. Kuna wanaume wanaweza kuja
kwako ukadhani ni wema lakini baada ya kumaliza haja zao
huwaoni, ndo maana huwa sioni haja ya kujilizaliza kwa mwanaume
coz akigundua umezimika ndo kabisa atakugeuza Toilet paper ya
kuchambia......
"Najua
wapo wengi sana wanaonitamani, lakini kwa taarifa yao ni kwamba
nipo makini sana na naitambua thamani yangu." Alisema Lulu.
Hata
hivyo Lulu alisema kuwa huwa anatongozwa na wanaume wengi
sana kutokana na uzuri alionao, hali inayomfanya abadili namba
ya simu kila mara kukwepa usumbufu.