post-feature-image
HomeBurudani

NILIJITEGEMEA KABLA SIJAKOMAA - CATHY:

KAMA kawa kama dawa, ndani ya Exclusive Interview leo tupo naye muigizaji mkongwe w...

JOKATE: HAKUNA KAMA DIAMOND
MSIBA WAKWAMISHA VIKAO VYA HARUSI YA ISABELA
BOB JUNIOR LIVE NA ‘MCHEPUKO’
KAMA kawa kama dawa, ndani ya Exclusive Interview leo tupo naye muigizaji mkongwe wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ambaye alianza sanaa tangu enzi za makundi hadi zilipofika zama za kurekodi sinema.
Muigizaji mkongwe wa sinema za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’
Alifanikiwa kuanza kutengeneza jina lake katika Kundi la Mambo Hayo na baadaye Kaole. Hapa chini amezungumza vitu vingi na mwandishi wetu, tujiunge naye:
Mwandishi: Umeanza kitambo sanaa, umri wako unaonekana ni mkubwa, je una miaka mingapi, kabila na umezaliwa wapi?

Cathy: Tafadhali sipendi kuanika mwaka wangu, ila mimi ni Mpare na nimezaliwa Kijiji cha Lembeni mkoani Kilimanjaro.
Mwandishi: Vipi kuhusu elimu yako?     Cathy: Elimu yangu ni ya kawaida sana, si kubwa ya kusema nikaajiriwe kwenye kampuni, kwanza siwezi kuajiriwa hata kwa mtu kwa sababu nina mambo mengi sana ya kufanya. Mwandishi: Kwa nini hutaki kuajiriwa?
Cathy: Mimi ni mtu wa kukimbizana na hela siwezi kukaa kwa mtu au kwenye ofisi nikisubiri mwisho wa mwezi.

Mwandishi: Wewe ni mtoto wa ngapi kwenu? Cathy: Mtoto wa nane katika familia ya mzee Rupia mwenye watoto 11, mimi na mwenzangu tulizaliwa mapacha.
Mwandishi: Cathy ni mtu wa aina gani? Cathy: Watu wanavyosema niko ni mcheshi, nina huruma sana, namwamini Mungu katika kila jambo, napenda amani, mtu wa watu napenda kujumuika na wenzangu bila kujali kipato, elimu kabila wala rangi, sidharau mtu yeyote na ndiyo maana niko kwenye vikundi vya kina mama wajasiriamali na vikundi hivi vina kila tabaka la watu.
Mwandishi: Jirani zako wanadai unajiona ni kweli? Cathy: Si kweli kila mtu Mtoni Kijichi (anapoishi) ni rafiki yangu, nawapenda na wao wananipenda sema huwezi kupendwa na kila mtu na mara nyingi watu wa hivyo huwa hawana sababu maalum ya kumchukia mtu ukimuuliza atakwambia , simpendi tu.
Mwandishi: Unapenda kitu gani katika maisha yako? Cathy: Napenda amani na kuambiwa ukweli pale ninapokosea kwani naamini nitakuwa nimejifunza kitu kipya na sitorudia kosa la kwanza.
Mwandishi: Wapare  wana sifa gani? Cathy: (Hapa anajivutia kwake) wapole sana na mara nyingi wamama wa Kipare ni wachapakazi ndiyo maana hata mimi nilipoanza kujitegemea sikuwa na shida kwani niliamini mafunzo ya kazi nilizopitia wakati niko nyumbani zilinifanya nijiamini kuwa naweza kuishi kwa kutegemea kazi ya mikono yangu.
Mwandishi: Ulianza kujitegemea ukiwa na umri gani?

Cathy: Kiukweli nilianza kujitegema nikiwa mdogo sana kama miaka kumi na kitu hivi, hata kumi na nane sikufikisha, nilikuwa bado sijakomaa kabisa.
Mwandishi: Daah! Ulikuwa mdogo sana, ulitoroka nyumbani au ulitoroshwa?
Usikose wiki ijayo kujua ili kujua sababu zilizomfanya Cathy ajitegemee akiwa na umri mdogo.

- gpl
Name

Burudani Habari Hot News Magazeti Majuu Michezo Teknolojia/Movie Track (Audio & Video)
false
ltr
item
Tabasam Blog: NILIJITEGEMEA KABLA SIJAKOMAA - CATHY:
NILIJITEGEMEA KABLA SIJAKOMAA - CATHY:
http://api.ning.com:80/files/QsQ1m7RyND3Q1o3RTC8IuLZ4w88zXcLT3YMNMkMXkKfwjVSCceV2zfb951UCklhZ2r3qCzGICaujmAViJRjWzUzYK-FlH7mR/paka.JPG
Tabasam Blog
https://tabasmtza.blogspot.com/2014/06/nilijitegemea-kabla-sijakomaa-cathy.html
https://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/
http://tabasmtza.blogspot.com/2014/06/nilijitegemea-kabla-sijakomaa-cathy.html
true
939923276739022787
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago