Vera Sadika ni jina la mrembo wa Kenya ambalo limekuwa sehemu ya mada kubwa nchini Kenya kutokana na uamuzi alioufanya wa kujichu...
Vera Sadika ni jina la mrembo wa Kenya ambalo limekuwa sehemu ya mada
kubwa nchini Kenya kutokana na uamuzi alioufanya wa kujichubua ngozi
yake ili afanane na wazungu.
Vera anaedaiwa kutumia pesa nyingi kuhudhuria clinic iliyomfanyia huduma hiyo.
Vera kabla na baada ya kujichubua
Wanawake wengi wa Kenya wammeendelea kumshambulia kwa uamuzi wake kwa
kuwa ngozi nyeusi ni sehemu ya uzuri wa mwanamke wa kiafrika na uamuzi
wake wa kuibadili ni kama kuukana Uafrika…kwa mujibu wa maoni hayo. Huku
kundi lingine kubwa la watumiaji wa twitter likimsakama.
Sadika ambaye anajulikana sana kwa vimbwanga vyake kwenye mitandao ya
kijamii na picha anazoshare akionesha jinsi alivyojaaliwa wezele
aliwajibu wanawake hao akidai huo ni uamuzi wake na anavyotaka kuufanyia
mwili wake huku akihoji kuwa Mzungu akijaribu kuwa mweusi hawasemi.
Mjadala huo wa Kenya umepelekea Vera kuwa maarufu zaidi na kupata
interview na vituo vya runinga vikubwa ikiwemo Al Jazeera na BBC.
Sadika Vera hakuishia hapo amepata nafasi kwenye gazeti kubwa na
kongwe la Marekani, New York Post ambalo limeandika habari inayomhusu na
kuipa kichwa cha habari kinachomtaja kuwa ni Kim Kardashian wa Kenya,
jina ambalo amekuwa akitajwa na baadhi ya watu nchini Kenya.